Waziri Mkuu Majaliwa Atangaza vita na watumishi wa Afya Wezi wa Dawa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuwachukulia hatua kali watumishi wa afya wanaojihusisha na wizi wa dawa katika hospitali.
kassim-1
Amesema hayo Jumapili hii mkoani Katavi akiwa na siku ya pili katika ziara yake mkoani humo ambapo alianza kutembelea kwenye hospitali ya wilaya ya Mpanda na kushuhudia changamoto ya dawa na vifaa tiba huku akiagiza kujengwa kwa duka la dawa ili kupunguza gharama.
Alitoa agizo kwa kila kiongozi kwenye eneo lake kuhakikisha kila dawa zinazopelekwa na serikali kwaajili ya kuwahudumia wananchi zinatumika kama ilivyokusudiwa.
“Nitairatibu vizuri nitamuita waziri wa afya aje hapa ili aje aone hii na wataalamu wake awaweke vizuri kwenye utawala wenu. Lakini pia na huduma ili huduma za hapa tuzipe hadhi ya kimkoamkoa tupate vifaa na tiba za kimkoa,” alisema.
“Nimepita huko ndani wengine wanaridhika na wanafarijika na huduma zenu vizuri muendelee, lakini wengine kidogo wananunua zile dawa ambazo haziko lakini kwa kuwa nyie mpo kwenye manispaa na vIjijini hadhi yenu na mgao wenu unakuwa mdogo kuliko kama mngekuwa kwenye ngazi ya mkoa ambapo sasa mnatibu kama mkoa,” aliongeza.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Jenarali mstaafu Raphael Muuga alisema ameshaunda tume juu ya huduma ya hospitali hiyo. “Nikatoa maelekezo kwamba tuwasiliane na MSD kuona mtiririko wa upatikanaji wa dawa”, alisema Muuga.
BY: Maukali music

No comments